MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (CCM), Dkt. John Magufuli amewaponda baadhi ya viongozi na wagombea wanaotoka vyama vya upinzani ambao wamekuwa wakiponda ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Chato, mkoani Geita ambako ndiko nyumbani kwao.
Magufuli amesema hayo leo wakati akizungumza na wananchi wa Chato katika kampenzi zake alizofanya kwenye Uwanja wa Mazaina na kuongeza kuwa haoni mtu mwingine anayegombea urais anaweza kufanya mambo aliyoyafanya hata robo.
“Ninyi watu wa Chato mna ushahidi mkubwa kwenye mambo ya miundombinu, kuna watu walikufa kwenye Bandari ya Chato hapa, pia ajali ya MV Bukoba, meli tulizozizoea kufanya safari zikapotea, baada ya miaka 20 tumekarabati meli zote na kununua nyingine mpya.
“Mtu anazungumza eti nimejenga Uwanja wa Ndege nyumbani (Chato), kwani nikifa nitakwenda nalo hilo liuwanja kaburini!? Lazima upange mipango mipana, tumejenga viwanja zaidi ya kumi na moja, Singida, Songea, Mtwara, Dodoma, hivyo vyote hawavioni wanakiona cha Chato tu, washindwe na wakalegee.
“Mtu anasema atagawa ubwabwa wakati hata kwake ubwabwa haumtoshi, mwingine anasema kula bata, hata misahafu inasema hakuna cha bure, msikubali kumpa mtu kwa kujaribu, mtajuta na mtakuja kuniambia. Mwingine anasimama ameshiba ugali anasema ndege hazina faida, huko alikotoka yeye amekuja na Bajaji mpaka hapa? Unajua mambo mengine yanaudhi.
“Kalemani anapambana umeme upo vijiji vingi, leo Chato ina umeme mtaani, Waziri Biteko anaomba umeme na Bukombe ni wilaya ya zamani kuliko Chato, nakuagiza Kalemani bado uwaziri unao, peleka taa za barabarani Bukombe.
