
Benki ya Akiba Commercial leo imezindua huduma ya malipo ya serikali ambapo sasa wateja wa benki hiyo wataweza kufanya malipo mbalimbali ya serikali kwenye benki hiyo kupitia akaunti yake ya Akiba Mobile.
Akizungumza na wanahabari makao makuu ya benki hiyo, Posta Jijini Jijini Dar, Meneja Mwandamizi Kitengo cha Maendeleo na Biashara wa benki hiyo, David Korosso amesema wamefikia kuanzisha huduma hiyo ili kutatua changamoto za wateja wao.

“Benki yetu ambayo imekuwa ikiwahudumia wateja wa chini na kati imekuwa ikifanya utafiti wa huduma zake na kuanzisha huduma mpya pindi wanapoona haja ya kufanya hivyo.
“Tumeamua kuanzisha huduma hiyo ambayo itawawezesha wateja wetu kufanya kwa haraka malipo mbalimbali kama vile huduma za Dawasco, Mamlaka ya Mapato (TRA), Bima ya afya, Faini za Trafiki malipo mengine.
“Tunazishauri taasisi binafsi na za serikali kufungua akaunti hiyo kwenye matawi yetu popote hapa nchini ili kuweza kupata huduma hiyo rahisi na ya haraka zaidi.

Katika kumalizia Korosso alisema benki inaendelea kutoa mikopo kwa wajasiriamali wadogo na kati na kuwataka wakafungue akaunti kwenye benki hiyo ili waweze kunufaika na mikopo hiyo na huduma nyinginezo.
HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL