×

Wahitimu Victory Sekondary Walivyoonesha Uskauti Mbele ya Wazazi

Wahitimu wakionesha ukakaaamavu walipokuwa kwenye mazoezi ya kiskauti.

Wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne katika shule ya Sekondari Victory iliyopo mkoani Pwani wameonyesha umahiri wao kwa kucheza michezo mbalimbali ikiwemo mafunzo ya kiskauti mbele ya mgeni rasmi, Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Pwani, Hildegard Makundi pamoja na wazazi na walezi waliohudhuria kwenye mahafali hayo.

Akizungumza wakati wa mahafali hayo ambayo ya kidato cha nne ambayo ni ya 13 mkuu wa shule hiyo, Ponsiano Mlelwa amesema kuwa wanafunzi hao wamepata mafunzo hayo kutoka kwa walimu waliobobea kwenye masomo ya michezo ambapo shule imewashirikisha wanafunzi katika program mbalimbali za kuwachangamsha kiakili ikiwemo michezo, midahalo na mengineyo.

“Pamoja na taaluma inayotolewa hapa pia kuna walimu wa michezo, watoto wanafundishwa mazoezi pamoja na mafunzo ya skauti ili kuweka miili yao kuwa imara na yenye afya.

Wakiwa kwenye zoezi la kumbeba kiskauti mwenzao aliyepata ajali.

“Watoto wametuonyesha namna ya kumsadia majeruhi aliyepata ajali kwa kutumia njia sahihi na kisha kumpa huduma ya kwanza kabla hajafikishwa kituo cha afya pia tumeona kwa ukakamavu walionao ambapo mmoja wao amevunja nondo kwa kutumia mikono.

“Pia tuna walimu wazuri wa masomo ya ujasiriamali ambao wamewafundisha watoto kutengeneza vitu mbalimbali ikiwemo sabuni za maji, za kuoshea vyombo, mafuta pamoja na dawa ya kusugulia choo zenye jina la Victory ambayo ndio lebo yetu.

“Kwa hiyo napenda kuwaomba wazazi waendelee kutupa ushauri sisi tutausikiliza na kuufanyia kazi ili tuweze kuongeza juhudi katika kuwapatia mafunzo yaliyo mema watoto wetu”. Alimaliza kusema.

Leave a Comment