×

Magufuli Amfariji Aliyekatwa Mapanga Msikitini – Video

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi,  John Magufuli,  ambaye pia ni mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho, amefika hospitali leo Ijumaa, Oktoba 2, 2020 kumfariji kiongozi wa CCM, Hamisi Nyange Makame maarufu kama Profesa Gogo (63),  ambaye alikatwa mapanga na wenzak wawili wakati wa swala ya alfajiri katika msikiti wa eneo la Kangagani wilayani Wete, mkoani Kaskazini, Zanzibar.

Magufuli amemtaka kiongozi huyo na CCM kwa jumla kutolipiza visasi, badala yake kuendelea kuwaombea waliotenda jambo hilo na Mungu atawalipa.

Aidha,  amewapongeza madaktari kwa juhudi zao kuokoa maisha ya kiongozi huyo na wenzake wawili huku akivitaka vyombo vya usalama kuwashughulikia wahusika wa matukio hayo na kuwafikisha kwenye mikono ya sheria ili sheria ichukue mkondo wake.


“Haiwezekani mtu unatoka msikitini unafika unakatwa panga, ni siasa zilizopitwa na wakati, kuna maisha baada ya siasa, kwa nini unapoelekea kushindwa unaanza kukata watu kwa mapanga, sasa ukishinda utawatawala akina nani?  Si wote utakuwa umewajeruhi?” amesema Magufuli.

 

Hali ya Profesa Gogo inaendelea kuimarika  vizuri.

 

Leave a Comment