
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe leo Oktoba 4, 2020 amesema mgombea wao wa Urais, Tundu Lissu hataendelea na kampeni kwa kipindi ambacho tume imezuia mikutano yake.
Amesema; “Tundu Lissu siyo tu ni mgombea wa Urais wa chama chetu, huyu ni Makamu Mwenyekiti wa Chama hivyo hatakosa cha kufanya kwa kipindi cha siku 7.
Chama kitampangia program mahususi kama Makamu Mwenyekiti kufanya majukumu ya kijamii na kisiasa.”-
Amesema, Watanzania hawatapata ujumbe wa mgombea wa Urais, lakini wataupata ule wa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA.
Pia Mbowe ameongeza; “Baada ya kushauriana kwa kina na mgombea wetu wa Urais Zanzibar, Said Mohammed ambaye alikuwa ameteuliwa awali na chama chetu, tumeona ni sahihi kabisa kwa chama chetu kumuunga mkono Seif Sharif Hamad, mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya ACT Wazalendo.”