×

Vodacom Yasherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja Ikitimiza Miaka 20

Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Vodacom, Harriet Lwakatare (kulia) akimshuhudia mmoja wa wateja wao akikata keki.

 Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom leo imesherehekea wiki ya Huduma kwa Wateja huku ikitimiza miaka 20 tangu kuanza kutoa huduma hapa nchini.

Akizungumza na wanahabari kwenye duka la Vodacom, Mlimani City Jijini, Dar Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo, Harriet Lwakatare amewapongeza wateja wao kwa kuendelea kuwa nao kwa kipindi chote hicho na kuwapongeza na watoa huduma wao kwa jinsi wanavyowahudumia wateja wao.

Harriet akigawa maua ya upendo wa wateja wao.

Harriet amesema watoa huduma wao wamekuwa wakitoa huduma kwa wateja hao kupitia maduka yao zaidi ya 530 yaliyopo nchi nzima.

Amesema pamoja huduma zinazotolewa kwenye maduka hayo pia wamekuwa wakitoa huduma kwa njia ya simu, kukutana ana kwa ana, kidigitali na njia nyinginezo.

Mambo ya shampeni nayo yalikuwepo.

Mkurugenzi huyo amesema kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele kuendena sambamba na maendeleo ya ulimwengu ili kuwapa wateja wao huduma bora.

“Miongoni mwa huduma tulizoziboresha hivi karibuni ni pamoja na mteja kujirudishia muhamala aliomtumia mtu mwingine kimakosa.

Harriet akigawa maua ya upendo kwa watoa huduma wa kampuni hiyo.

“Si hilo tu sasa hivi hata kama mteja atakuwa amesahau namba ya siri ya PUK yake ataweza kujihudumia mwenyewe”. Amesema Harriet.

Baada ya kusema hayo, mkurugenzi huyo amewakaribisha wateja wao kwenye maduka yao mbalimbali ili kama kuna changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo waweze kutatuliwa.

Mambo yakiendelea dukani hapo.

Uzinduzi huo ulipomalizika Harriet alitumia nafasi hiyo kuwalisha keki na kuwanywesha shampeni wateja na watoa huduma wa kampuni hiyo waliokuwa dukani hapo.

Leave a Comment