×

Benki ya Akiba Ilivyoungana na Wateja Kuzindua Wiki ya Huduma kwa Wateja

Mjasiriamali Boaz Magito (kulia) akimshukuru Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Akiba, Dora Saria ambaye benki yake imemuwezesha kufikia mafanikio makubwa katika biashara zake ikiwemo duka lake la dawa za mifugo lililopo Tegeta Dar.

Benki ya Akiba Commercial imezindua wiki ya huduma kwa wateja katika hafla iliyofanyika tawi lao la Tegeta jijini Dar kwa kuungana na wateja wao katika maadhimisho hayo.

Katika uzinduzi huo maofisa wa benki hiyo walizungumza na wateja wao kwenye tawi hilo na wengine kuwatembelea kwenye biashara zao.

Muonekano wa duka la mjasiriamali huyo kwa nje.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Benki ya Akiba Commercial, Dora Saria amesema dhumuni kubwa la hafla hiyo ni kuwashukuru wateja pamoja na watoa huduma wao.

Baada ya uzinduzi huo maofisa wa benki hiyo walikata keki pamoja wateja wao na kisha kupata brekfast ya pamoja katika kuonesha mshikamano na upendo walionao kwao.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa benki hiyo, Innocent Ishengoma akiweka mambo sawa.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Dora alisema;

“Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja tumeamua kuwapa zawadi mbalimbali wateja wetu walioshinda katika zoezi la kuweka akiba kubwa zaidi.

“Pia katika wiki hii ya Huduma kwa Wateja tumezindua tena kampeni ya kujiwekea akiba hivyo tunawashauri wananchi wote kufungua akaunti Benki ya Akiba na kushiriki katika zoezi hilo ili nao waweze kufaidikia na huduma hiyo.

Sehemu ya wahudumu wa tawi la Tegeta wakiwa kwenye picha ya pamoja katika kufurahia maadhimisho hayo.

“Pamoja na kuwapa zawadi wateja wetu pia tumetambua na mchango wa staff wetu ambapo tumeangalia idara mbalimbali na kuteua wafanyakazi bora katika kila idara na kuwatunukia vyeti ili nao waone jinsi taasisi wanayofanyia kazi jinsi inavyowathamini”. Alisema Dora.

Katika kumalizia Dora amesema benki yao imeanzisha huduma ya malipo ya serikali ambayo inaitwa Akiba Mobile.

Watoa huduma wa benki hiyo wakiserebuka kwaito kufurahia maadhimisho hayo.

Kupitia huduma hiyo mteja wa benki hiyo ataweza kufanya malipo mbalimbali ya serikali kama vile faini za trafiki, kulipia leseni, kodi za majengo na malipo mengine ya serikali. Alimaliza kusema. HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL

Leave a Comment