×

Vodacom Yafanya Jambo Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA)

Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Vodacom, Harriet Lwakatare (kulia) na Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Paul Rwegasha wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka hilo.

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom imeamua kufanya jambo kwa kuwafungulia duka wateja wa kampuni hiyo katika eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Harriet akikata keki.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa duka hilo, Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Vodacom, Harriet Lwakatare amesema wameamua kufungua duka hilo kwa ajili ya kuwasaidia wateja wao wa maeneo hayo.

Shampeni nazo zilibatuliwa kusherehekea uzinduzi huo.

“Hili eneo lina pilikapilika nyingi ikiwemo abiria wanaoingia na kutoka hapa nchini ambapo wanahitaji huduma ya uhakika wa mawasiliano.

“Hivyo basi tumeona ni viuzuri tukiwawekea duka letu hapa ili waweze kutatua changamoto ya kimawasiliano”. Alisema Harriet.

Harriet akizungumza na watoa huduma wao kampuni hiyo baada ya kuwatangaza kuwa watoa huduma bora.

Baada ya kusema hayo, Harriet aliwaongoza watoa huduma wa kampuni hiyo kukata keki na kufungua shampeni wakisherehekea uzinduzi wa duka hilo pamoja na kusherehekea wiki ya Huduma kwa Wateja.

Harriet akimkabidhi zawadi mteja wao katika kusherehekea wiki ya huduma kwa wateja.

Katika hafla hiyo, Harriet aliwapa zawadi watoa huduma bora kwa kampuni hiyo na kuwahamasisha wengine kujituma zaidi ili nao taasisi wanayofanyia kazi iwazawadie kama wenzao hao.

Leave a Comment