×

DKT JPM Alivyowapigia Debe Wagombea Ubunge wa CCM Dar

Mgombea wa kiti cha urais kupitia CCM Dkt. John Pombe Magufuli jana aliwaomba wananchi wamchague tena amalizie awamu yake ya pili ili azidi kufanya maendeleo zaidi ya aliyoyafanya.

Dkt. Magufuli aliwaomba wanachi ridhaa hiyo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar ambapo katika mkutano huo, aliwanadi wagombea ubunge pamoja na udiwani katika mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Benjamini Mkapa Dar.

Dkt. JPM aliwaasa wakazi wa jiji la Dar kuwachagua wabunge hao ili akashirikiane nao vizuri katika kuzidi kuriboresha jiji la Dar ambalo ndani ya kipindi cha miaka mitano ameshafanya mambo makubwa ya kimaendceleo ambayo hayajawahi kutokea.

Akimnadi Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Profesa Kitila Mkumbo.
Jerry Slaa Jimbo la Ukonga.
Mussa Azzan Zungu Jimbo la Ilala.
Issa Jumanne Mtemvu Jimbo la Kibamba.
Bona Ladislaus Kamori Jimbo la Segerea.
Dkt. Faustine Ndugulile Jimbo la Kigamboni.
Josephat Gwajima Jimbo la Kawe.
Doroth Kilave Jimbo la Temeke.                                                                                                            HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL   

Leave a Comment