×

Ahukumiwa Kifo Baada ya Kuua ‘Makahaba’ Tisa – Video

MTU mmoja, Gracious David-West (26), amehukumiwa kifo baada ya kukiri kuwanyonga wanawake tisa nchini Nigeria.

 

Gracious aliyewaua wanawake hao kwa nyakati tofauti, kesi yake iliibua ghadhabu kubwa ambapo hukumu hiyo imetolewa katika mji wa Kusini wa Port Harcourt.

 

Waendesha mashtaka wamesema mwanamme huyo aliwanyonga wanawake hao ambao wanadaiwa kufanya biashara haramu ya kuuuza miili yao (makahaba) katika hoteli mbalimbali nchini Nigeria alikokuwa akikutana nao kati ya mwezi Julai na Septemba 2019.

Jaji Adolphus Enebeli amesema kifo chake kitatekelezwa kwa kunyongwa licha ya hukumu hiyo ya kifo ni nadra sana kutolewa nchini Nigeria na hukumu kama hiyo kwa mara ya mwisho kutolewa ilikuwa ni mwaka 2016 kwa watu watatu.

 

Mmoja wa waathirika alinusurika na shambulio hilo lakini hakuwa miongoni mwa waliotoa ushahidi wakati kesi hiyo inaendelea.

Aidha, Serikali ya Nigeria imesema kwamba mwathirika huyo hajulikani alipo licha ya kuombwa asitoroke. Polisi imesema mshtakiwa pia naye alikiri kutekeleza mauaji ya wanawake wengine sita.

 

Mamlaka inasema mauaji hayo yalitokea baada ya mtuhumiwa kufanya ngono nao na baada ya hapo aliwanyonga kwa kutumia shuka jeupe.

Mwanzoni mwa kesi hiyo mtuhumiwa alikiri kuwa na hatia lakini jaji alitaka kesi hiyo kuendelea kusikilizwa kutokana na uzito wa uhalifu. Kwa muda, mamlaka iliisitisha na kutafuta ushahidi ambao ulisikilizwa mahakamani.

 

Polisi wanasema David West alikuwa akiwaua wanawake mwenyewe bila ushirika na mtu. Wakati wa mfululizo wa mauaji ya wanawake hao mwezi Septemba mwaka jana, raia wenye hasira waliandamana barabarani na kuitaka mamlaka kuchukua hatua kutatua tatizo hilo.

Mtuhumiwa alikamatwa Septemba 19, wakati akijaribu kuondoka Port Harcourt. Picha za video za CCTV zilimpiga picha akiwa anaondoka hotelini na picha hizo zilienea katika mitandao ya kijamii.

 

Watu wa usalama walimkuta katika basi akisafiri kutoka Uyo katika jimbo la Akwa Ibom ambako ni umbali wa dakika 45 kutoka Port Harcourt. David-Westa alizaliwa katika mji wa wavuvi wa jimbo la Buguma, eneo ambalo linafahamika sana kwa kutengeneza mafuta na fukwe zake kuwa za kuvutia.

 

View this post on Instagram

 

Mtu mmoja Gracious David-West (26) amehukumiwa kifo baada ya kukiri kuwanyonga wanawake tisa nchini Nigeria. Gracious aliyewaua wanawake tisa na kesi yake ikaibua ghadhabu amehukumiwa kunyongwa katika mjini wa Kusini wa Port Harcourt. Waendesha mashtaka wamesema mwanaume huyo aliwanyonga wanawake hao katika hoteli mbalimbali nchini Nigeria alikokuwa anakutana nao kati ya mwezi Julai na Septemba 2019. Jaji Adolphus Enebeli amesema kifo chake kitatekelezwa kwa kunyongwa. Hukumu hiyo ya kifo ni nadra sana kutolewa nchini Nigeria na hukumu kama hiyo kwa mara ya mwisho kutolewa ilikuwa ni mwaka 2016 kwa watu watatu. Mmoja wa waathirika alinusurika na shambulio lake lakini hakuwa miongoni mwa waliotoa ushahidi wakati kesi hiyo inaendelea. Aidha, Serikali ya Nigeria imesema kwamba mwathirika huyo hajulikani alipo licha ya kuombwa asitoroke. Polisi imesema mshtakiwa pia naye alikiri kutekeleza mauaji ya wanawake wengine sita. Mamlaka inasema mauaji hayo yalitokea baada ya mtuhumiwa kufanya ngono nao na baada ya hapo aliwanyonga kwa kutumia shuka jeupe.Waathirika walikuwa wanafanya kazi ya kujiuza miili yao. Mwanzoni mwa kesi hiyo mtuhumiwa alikiri kuwa na hatia lakini jaji alitaka kesi hiyo kuendelea kusikilizwa kutokana na uzito wa uhalifu. Kwa muda, mamlaka iliisitisha na kutafuta ushaidi ambao ulisikilizwa mahakamani. Polisi wanasema David West alikuwa akiwaua wanawake mwenyewe bila ushirika na mtu Wakati wa mfululizo wa mauaji ya wanawake hao mwezi Septemba mwaka jana, raia wenye hasira waliandamana barabarani na kuitaka mamlaka kuchukua hatua kutatua tatizo hilo. Mtuhumiwa alikamatwa Septemba 19, wakati akijaribu kuondoka Port Harcourt wakati ambapo mamlaka ilikuwa karibu kumkuta na hatia. Picha za video za CCTV zilimpiga picha akiwa anaondoka hotelini na picha hizo zilienea katika mitandao ya kijamii. Watu wa usalama walimkuta katika basi akisafiri kutoka Uyo katika jimbo la Akwa Ibom , ambako ni mbali kutoka Port Harcourt kwa dakika 45. David-Westa alizaliwa katika mji wa wavuvi wa jimbo la Buguma, eneo ambalo linafahamika sana kwa kutengeneza mafuta na fukwe zake kuwa za kuvutia. #globalhabariupdates

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

Leave a Comment