Msanii wa Bongo Fleva, Queen Darleen, na mumewe, Isihaka, wamepata mtoto wa kike ambaye wamempa jina la Balqis Isihaka.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Darleen ambaye ni dada wa Diamond Platnumz amethibitisha kuwa amejifungua salama na kupost picha ya mtoto wao kisha kuandika maneno machache ya kumshukuru Mungu kwa zawadi hiyo ya kipekee.
Nasi Global Publishers tunamtakia maisha marefu na yenye afya tele mtoto Balqis, Mungu amlinde na amtunze zaidi na zaidi.
Hongereni Darleen na Isihaka.


