×

Waholanzi kumleta Kaze Yanga sc

IMEBAINIKA kuwa wakati Mrundi Cedric Kaze, akijiandaa kuja kuchukua mikoba ya kuwa kocha mkuu wa Yanga, Waholanzi ndiyo ambao watahusika kumleta kocha huyo hapa nchini.

 

Waholanzi hao kupitia Shirika la Ndege la taifa hilo, KLM Royal Dutch Airlines (KLM), ndiyo watakaombeba Kaze kwa kumtoa Canada alipo kwa sasa na kumshusha katika ardhi ya Tanzania Alhamisi saa 4 usiku, maalum kuanza kazi kwenye kikosi hicho.

 

Kaze anatua Bongo kwa ajili ya kuungana na Yanga baada ya timu hiyo kusitisha mkataba wa Mserbia, Zlatko Krmpotić ambaye alikuwa kocha mkuu wa timu hiyo.

 

Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM ambao ni wadhamini wa Yanga, Injinia Hersi Said, amesema ndege hiyo ya KLM ndiyo ambayo itahusika kumshusha kocha huyo hapa nchini. “Kocha atafika na ndege ya KLM, siku ya Alhamisi saa 4 usiku kwa ajili ya kuanza kazi,” alisema kwa kifupi Hersi.

Said Ally, Dar es Salaam

Leave a Comment