
Taswira ya daraja la sasa la Wami linalotumika lenye urefu wa mita 88.75, lililopo mkoani Pwani. Daraja hilo ni kiungo muhimu kati ya Chalinze na mikoa ya kaskazini na nchi jirani.

Mwonekano wa hatua za ujenzi wa daraja jipya la Wami ambalo litakuwa na urefu wa mita 510 na upana wa mita 11.85 na barabara unganishi zenye urefu wa kilomita 3.8 ukiendelea mkoani Pwani.
KAZI ya ujenzi wa nguzo za daraja jipya la Wami inaendelea mkoani Pwani ambapo umefikia asilimia 45 na unagharimu takribani kiasi cha shilingi bilioni 67.8 ukitarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Septemba 2021.
