WAKATI klabu ya Yanga ikiwa imefunga jumla ya mabao saba ndani ya ligi baada ya kucheza mechi tano, mzawa Deus Kaseke amekuwa ni nyota wa kwanza kuhusika moja kwa moja kutengeneza nafasi ya bao.
Kwenye mabao saba ambayo yamefungwa, wageni wamehusika kwenye jumla ya mabao sita ambapo Michael Sarpong raia wa Ghana alifunga bao la kwanza ndani ya Yanga ilikuwa mbele ya Tanzania Prisons, Lamine Moro raia wa Ghana alifunga mabao mawili ilikuwa mbele ya Mbeya City na Mtibwa Sugar kwa pasi za Carlos Carlinhos raia wa Angola.
Tonombe Mukoko, alifunga bao dhidi ya Kagera Sugar kwa pasi Tuisila Kisinda wote wakiwa ni raia wa Congo, Haruna Niyonzima wa Rwanda alifunga bao lake la kwanza mbele ya Coastal Union baada ya kipa kutema mpira, Yacouba Songne raia wa Burkina Faso alifunga bao la kwanza kwa pasi ya Mukoko.
Kaseke aliweza kufanya hivyo kwa kutoa pasi yake ya kwanza kwa Carinhos, Uwanja wa Mkapa wakati Yanga ikishinda kwa mabao 3-0 ilikuwa Oktoba 3.
Lunyamadzo Mlyuka, Dar es Salaam
