×

Mawakala Wanne Chadema Wafariki Ajalini

WATU  wanne ambao ni mawakala wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa, katika ajali ya gari iliyotokea leo Oktoba 21, 2020 kijiji cha Malonji, Sumbawanga, mkoani Rukwa.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Justine Masejo, amethibitisha  kuwa watu watatu wamefariki hapohapo na mmoja amefariki akiwa hospitali na majeruhi wanaendelea na matibabu akiwemo dereva ambaye yupo chini ya ulinzi.

 

Ameongeza kuwa gari iliyopata ajali ni Noah yenye namba za usajili T 381 DZQ,  chanzo cha ajali kikiwa ugeni wa dereva kwenye barabara hiyo na kuendesha gari kwa kasi hivyo kumshinda kwenye kona na kusababisha ajali hiyo.

Leave a Comment