×

Mdose: Kitakachoikuta E- Media Watasimulia

BEKI wa kati wa kutegemewa ndani ya kikosi cha Global FC, Omary Mdose, ameeleza kuwa wameshanoa makali yao tayari kwa mapambano ya mchezo wa kirafi ki utakaochezwa leo Ijumaa dhidi ya kikosi cha E – Media.

 

Global FC na E Media, leo Ijumaa majira ya saa 10:00 jioni, watapambana kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers jijini Dar. Global FC katika mechi tisa za hivi karibuni, imeshinda sita, sare mbili na kupoteza moja.

 

Mdose aliliambia Championi Ijumaa kuwa: “Maandalizi yapo vizuri, tumejiandaa kuibuka na ushindi mnono kwani tuna kikosi imara kuanzia wachezaji wanaoanza mpaka wanaokaa benchi.

 

Pia tuna benchi la ufundi imara chini ya kocha wetu Philip Nkini.“Kwa kweli E Media watakachokutana nacho nadhani watawasilimua wengine ambao wamekuwa wakiomba kucheza na Global. Tutawafunga mpaka waseme basi.”

 

Naye kiungo mshambuliaji wa wa Global FC, Abdulghafal Ally ‘Grealish’, amesema kuwa makosa madogomadogo yaliyojitokeza kwenye mchezo uliopita ambao walipoteza, Kocha Nkini ameshayafanyia kazi, hivyo wanaenda kupambana ili kurudisha furaha kwa mashabiki wao.

Stori na Manjiro Lyimo

Leave a Comment