Dakika 90 za Mchezo Kati ya Manchester City na Aston Villa kwenye Uwanja wa Wembley zimemalizika huku Manchester City wakiibuka Mabingwa wa Carabao Cup kwa msimu wa tatu mfululizo baada ya kuichapa Aston Villa 2-1.
Hata hivyo, Mtanzania Mbwana Samatta amekuwa mchezaji wa kwanza wa Tanzania kuifunga goli Manchester City na amekuwa mchezaji wa tano kutoka Bara la Afrika kufunga kwenye Kombe la Ligi, wengine ni Didier Drogba , Joseph-Désiré Job, Obafemi Martins na Yaya Touré.
Samatta amefunga bao dakika ya 41 akiunganisha kwa kichwa cha kupiga mbizi baada ya kupokea pasi toka kwa Anwar El- Ghazi. Man City walikuwa wa kwanza kufunga bao kupitia kwa mshambuliaji wao Sergio Aguero dakika ya 20 na kiungo Rodri kufunga la pili dakika 34.

