POLISI mkoani Shinyanga wanamshikilia mgombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa tiketi ya (CHADEMA), Salome Makamba, kwa tuhuma za kufanya fujo, kuchana karatasi za matokeo ya kura na kumjeruhi msimamizi wa uchaguzi katika kituo cha kuhesabia kura cha Shule ya Msingi Bugweto “B”.
Mkuu wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Debora Magiligimba, amethibitisha kumshikilia mgombea huyo: “Baada ya matokeo kukamilika kujumlishwa, alipewa karatasi ya matokeo kuyasoma, nadhani hakuridhika nayo aliamua kuichana karatasi ya matokeo hayo na kumshambulia msimamizi wa uchaguzi katika kituo hicho na kumjeruhi mguu….
“Hivyo tunamshikilia kwa ajili ya upelelezi, ukikamilika tutamfikisha mahakamani. Sisi Jeshi la Polisi Shinyanga tumejipanga kwa yeyote atakayetaka kuleta vurugu au uvunjifu wa amani tutamshughulikia kwa mujibu wa sheria,” amesema Magiligimba.
