×

Mwinyi Aapishwa Rais wa Zanzibar – Video

 

ALIYEKUWA rais mteule  wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi, leo Novemba 2, 2020, ameapishwa  kuwa rais wa awamu ya nane wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika Uwanja wa Amani Visiwani Zanzibar.

Mwinyi alitangazwa mshindi wa nafasi ya urais Zanzibar katika uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita kwa asilimia 76. 27% huku mpinzani wake Maalim Seif akiwa mshindi wa pili kwa asilimia 19.87%.

Aliyekuwa rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, alitangaza kuwa siku leo ni mapumziko ili watu wote Zanzibar waweze kushiriki kwa ukamilifu sherehe hizo.

Akizungumza baada ya kuapishwa, Mwinyi amesema anatambua wajibu unaoambatana na dhima ambao ni kuwaongoza Wazanzibar kwa misingi ya haki, uadilifu na usawa bila ya kubagua mtu yeyote kutokana na itikadi yake, jinsia, dini au eneo analotoka.
“Nawashukuru wananchi kwa kutumia haki yenu ya kikatiba ya kupiga kura na kuwachagua viongozi wenu kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, kujitokeza kwenu kwa wingi katika kupiga kura ni kielelezo cha kukomaa kwenu kisiasa na kidemokrasia.
“Rais Magufuli ameniagiza nifikishe salamu zake za pongezi kwa Wazanzibar wote kwa kufanikisha uchaguzi wetu kwa usalama na kushiriki kwa wingi katika shughuli hii ya kumuapisha rais mpya. Kujitokeza kwenu kwa wingi kupiga kura ni kielelezo cha kukomaa kwenu kisiasa na kidemokrasia na kutambua kuwa uchaguzi ndiyo njia sahihi ya kupata viongozi wa nchi yetu kwa misingi ya sheria na katiba.
“Kama nilivyozungumza wakati wa kupokea matokeo ya uchaguzi leo naomba nirudie kuwa lengo letu ni kuijenga Zanzibar.   Zanzibar mpya inajengwa na sisi sote, bila kujali tofauti zetu za kiitikadi. Serikali nitakayoiunda itaongozwa kwa misingi ya haki, uwajibikaji, uwazi na usawa kwa wananchi wote bila ya kubagua mtu yeyote kutokana na itikadi yake, jinsia au eneo analotoka, kwani sote ni wamoja.
“Zanzibar mpya itajengwa na sisi sote bila kujali tofauti zetu za kiitikadi, ninawaahidi niko tayari kuyaendeleza maridhiano yaliyo katika katiba yetu.   Zanzibar ni kubwa na ni muhimu kuliko tofauti zetu.
“Ninawaahidi niko tayari kuyaendeleza maridhiano yaliyo katika katiba yetu na kushirikiana nanyi kuijenga Zanzibar mpya.   Zanzibar ni kubwa na muhimu kuliko tofauti zetu,” amesema.

Leave a Comment