×

CCM Yatangaza Nafasi za Spika, Meya

BAADA ya kukamilika kwa uchaguzi mkuu, Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho kimepata ushindi mkubwa kimewaalika wanachama wa chama hicho wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali za vyombo vya uongozi ikiwa ni pamoja na nafasi ya spika na naibu spika wa Bunge la Tanzania.

 

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya chama hicho (NEC) – Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole,  amesema nafasi nyingine ambazo wanachama wanaweza kuomba ni pamoja na meya wa halmashauri ya jiji au manispaa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya.

 

“Msisitizo unawekwa kwamba sambamba na sifa stahiki kwa mujibu wa sheria za nchi, waombaji wote lazima wawe wamekidhi sifa za uongozi,” imeeleza taarifa hiyo.

 

Tarehe ya kuchukua na kurejesha fomu kwa nafasi zote tajwa ni leo Novemba 2, 2020 na Novemba 3, 2020.

 

Leave a Comment