×

Uganda: Museveni Apitishwa Kuwania Urais

RAIS Yoweri Museveni amepitishwa na Tume ya Uchaguzi Uganda kuwa mgombea wa urais kupitia chama tawala cha NRM katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Februari mwaka 2021.

 

Museveni amekuwa madarakani tangu mwaka 1986, amesema:  “Nashukuru kwa uteuzi, naambiwa kuna wanaotaka kuanzisha machafuko; hakuna wa kuitishia Uganda kwa machafuko, watafeli, tulinde amani”.

 

Kiongozi huyo atachuana vikali na msanii Bobi Wine ambaye jina lake limepitishwa kuingia katika kinyang’anyiro hicho.

Leave a Comment