×

Rais Magufuli Awashukuru Watanzania

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mhe.Mama Janeth Magufuli leo ameshiriki misa ya Dominika ya 32 ya mwaka A katika Parokia ya Mtakatifu Bikira Maria Imaculata Chamwino.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Sakramenti Takatifu toka kwa Padre Paul Mapalala wakati wa Misa ya Dominika ya 32 Mwaka “A” katika Parokia ya Bikira Maria Imakulata Chamwino Ikulu Dodoma leo Jumapili Novemba 8, 2020.

Mhe.Rais Magufuli amewashukuru wa Tanzania kwa kuendelea Kuwa na imani nae kwa kumchagua tena katika uchaguzi wa mwaka huu na kuwaomba kuendelea kumuombea kwa Mwenyezi Mungu.

aidha amewashukuru Waumini wa Madhehebu mengine ya Dini waliojitokeza kuchangia ujenzi wa Msikiti ,amebainisha kuwa kitendo hicho kinadhihirisha umoja, upendo na mshikamano wa dhati walionao Watanzania.

Leave a Comment