×

Ujenzi wa Vyoo Kwenye Mikusanyiko Waanza Simiyu

Wachimbaji wa madini katika mgodi wa Dutwa wilayani Bariadi mkoani Simiyu ni baadhi ya walengwa wa huduma hiyo ya vyoo.

 

ILI kuepuka na magonjwa ya mlipuko katika kipindi hiki cha mvua za vuli, Serikali ya wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu imeanza ujenzi  yoo, katika machimbo ya madini mkoani humo na minada ambayo hukusanya idadi kubwa ya watu kutoka ndani na nje ya milaya hiyo.

Hatua hiyo imetokana na agizo la Mkuu wa Wilaya hiyo, Festo Kiswaga alilolitoa wakati akizungumza na waandisi wa habari mkoani Simiyu.

Alisema katika kipindi hiki cha mvua, lazima maeneo yenye mikusanyiko na idadi kuwa ya watu kujengwe vyoo vya kutosha ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko.

Kiswaga alisema magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu yanaweza kuzuilika kama masharti ya usafi yatazingatiwa na kwamba ujenziwa vyoo ni lazima katika maeneo hayo na sio matakwa ya mtu binafsi.

“Kunzania sasa katika kipindi hiki ambacho tunataraji kutakuwa na mvua za mfululizo, lazima mashariti ya afya yazingatiwe. Moja ya jambo kubwa ambalo kuanzia sasa nataka litekelezwe ni ujenzi wa vyoo kwenye minada na machimbo yetu ya madini kule Gasuma na maneneo mengine,”aliusema Kiswaga na kuongeza;

“Nilitoa maelekezo nashukuru kwamba yameanza kutekelezwa. Naamini Bariadi itakuwa salama na hatutakuwa na magonjwa ya mlipuko kama Kipindupindu na Mengine.”

Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Afisa Afya wa Mkoa wa Simiyu, Ruben Malimi alisema walipokea maagizo ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi na kwamba wameyafanyia kazi kwa asilimia mia moja na ujenzi wa vyoo huo umetekelezwa.

“Nikweli Mkuu wa Wilaya ya Bariadi aliagiza ujenzi wa vyoo ufanyike katika mikusanyiko ya watu ikiwemo minada na machimbo ya madini. Tumetekeleza hilo ka asilimia miamoja. Hili jambo ni muhimu kwetu sote kwani tutaweza kuepukana na magonjwa ya milipuko hasa katika nyakati hizi za mvua,”alisema Malimi

Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Simiyu waliyozungumza na Mwandishi Wetu walisema kuwa hiyo ni hatua njema, kwani nyakati za mvua magonjwa mengi hutokea hasa kipindupindu.

“Mimi binafsi kama mkazi wa Bariadi ili naona ni jambo jema, ujenzi wa vyoo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuepukana na magonjwa ya milipuko nampongeza Mkuu wa Wilaya na Idara yake ya afya,”alisema Mandu Maduhu Mkazi wa Gasuma Bariadi

NA MWANDISHI WETU

 

Leave a Comment