×

SBL Yadhamini Mashindano ya Waitara Golf Kupitia Kinywaji cha Johnnie Walker

Mkurugenzi wa masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Mark Mugisha akizungumza na wachezaji wa Klabu ya Gofu ya Lugalo jijini Dar es Salaam watakaoiwakilisha klabu hiyo katika mashindno ya TPC Open yanayofanyika mjini Moshi muda mfupi baada ya SBL kutangaza udhamini wa mashindano ya gofu ya Waitara ya mwaka huu kupitia kinywaji cha Johnnie Walker.

TAKRIBANI wachezaji 150 wa golf kutoka sehemu mbali mbali hapa nchini wanatarajia kuchuana vikali kwenye mashindano ya kila mwaka maarufu kama  Waitara Golf Tournament, yanayodhaminiwa na kinywaji cha Johnnie Walker (JW) kinachosambazwa na kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL)

Mwaka jana, mashindano haya yanayojizolea umaarufu mkubwa, yalidhaminiwa pia na kampuni ya SBL kupitia bia yake ya Serengeti Lite.

Akitangaza udhamini huo mbele ya waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Mark Mugisha alisema udhamini wa JW kwenye mashindano hayo unalenga kukuza na kuendeleza mchezo wa gofu.

“SBL kupitia kinywaji cha kimataifa cha Johnnie Walker inayofuraha kuwa mdhamini wa mashindano ya Waitara Golf Tournament kwa mwaka huu. Udhamini huu unaonyesha nia yetu ya kusaidia maendeleo ya michezo hapa nchini,” alisema Mark

Mkurugenzi wa masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Mugisha(kulia) akiteta jambo na mwenyekiti wa Klabu ya Gofu ya Lugalo Brigedia Jenerali mstaafu Michael Luwongo (katikati) muda mfupi baada ya kampuni ya SBL kutangaza udhamini wa mashindano ya gofu ya Waitara ya mwaka huu jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni nahodha wa Klabu hiyo kepteni Japhet Masai.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa mashindano hayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka kuanzia mwaka 2006, na hivyo mashindano yaliyoanza muda mrefu zaidi hapa Tanzania na kuongeza kuwa JW inayofuraha kuwa sehemu ya mashindano hayo makongwe.

“Wakati tukishereheka miaka 200 tangu kuanza kutengenezwa kwa JW ambayo kwa sasa ni wisky namba moja ulimwenguni, tunayofuraha kusafiri katika miaka yote hii tukiendelea kuwa imara na katika ubora ule ule,” alisema.

Mwenyekiti wa Klabu ya Gofu ya Lugalo Brigedia Jenerali mstaafu Michael Luwongo (wa pili kulia) akifurahia zawadi ya kinywaji cha Johnnie Walker alichopewa na Mkurugenzi wa masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Mark Mugisha(kulia) muda mfupi baada ya baada ya kutangazwa udhamini huo. Kushoto ni nahodha wa Klabu hiyo, kepteni Japhet Masai na meneja masoko wa Johnnie Walker Minga Lumuli.

Johnnie Walker ni moja kati pombe kali zenye ubora wa hali ya juu na hadhi ya kimataifa. Kinywaji hiki kina jumla ya aina tano ambazo zimeshinda tuzo za ubora wa kimataifa. Aina hizo ni pamoja na JW Red Label, JW Black Label, JW Green Label, JW Gold Label, na JW Blue Label kila moja ikiwa na historia yake ya kipekee.

Kwa upande wake mwenyekiti wa klabu ya Gofu ya Lugalo Brigedia Jenerali mstaafu Michael Luwongo aliishukuru SBL kupitia JW kwa kukubali kudhamini mashindano hayo na kuyataka makampuni mengine kujitokeza kusaidia mchezo wa gofu.

Nahodha wa Klabu ya Gofu ya Lugalo, Kepteni Japhet Masai akiongea na waandishi wa habari baada ya SBL kutangaza udhamini wa mashindano hayo. Kulia ni Mkurugenzi wa masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Mark Mugisha na ayefuatia ni mwenyekiti wa Klabu ya Gofu ya Lugalo Brigedia Jenerali mstaafu Michael Luwongo.

“Tunaishukuru sana kampuni ya SBL kwa muendelezo wao wa kufadhili mashindano haya na mchezo wa gofu kwa ujumla. Kwa sasa tunaweza kusema SBL ndiyo mdhamini mkubwa wa mashindano haya,” alisema Brigedia Jenerali Luwongo.

Leave a Comment