×

Rais Mwinyi Kutangaza Baraza la Mawaziri Kesho Nov. 19

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi kesho, Novemba 19, 2020, anatarajiwa kutangaza baraza  la mawaziri  katika hafla maalum itakayofanyika asubuhi.

 

Dkt. Mwinyi ameshamteua Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi Talib Haji.

 

Pia, ameshamteua Mkurugenzi Mkuu wa Shirika Ia Bandari Zanzibar, Nahaat Mohammed Mahfoudh na Katibu wa Rais, Suleiman Ahmed Salch.

 

Katika hatua nyingine Mwinyi amefanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya Mnazi Mmoja na kuutaka  uongozi wa hospitali hiyo  kuhakikisha watendaji wake wote wanatambulika kwa majina mara moja  ili wanaokwamisha huduma wajulikane.

 

Akizungumza mara baada ya ziara hiyo, ameweka wazi kuwa ujio wake katika hospitali hiyo umetokana na  taarifa kutoka kwa baadhi ya wagonjwa wanaofika kwenye hospitali  hiyo ambao wanalalamika juu ya kutoridhishwa na huduma zinazotolewa hospitalini hapo.

Leave a Comment