×

Familia ya George Floyd Kulipwa Bilioni 63


Baraza la #Minneapolis limeidhinisha makubaliano ya kuilipa familia ya George Floyd kiasi cha dola milioni 27 (takriban Tsh. Bilioni 63) ikiwa ni karibu mwaka mmoja tangu Mmarekani huyo Mweusi alipouliwa na Polisi.

Hicho ni kiasi kikubwa zaidi cha fedha kuwahi kulipwa kwa familia za Wahanga wa Matendo ya Ukatili yanayofanywa na Polisi na malipo hayo yanaondoa uwezekano wa familia ya Floyd kufungua kesi Mahakamani.

Floyd alifariki Mei 2020 baada ya Polisi mzungu kumkandamiza kwa goti shingoni kwa zaidi ya dakika 8 tukio ambali lilirekodiwa na mpita njia. Kifo chake kilizusha maandamano makubwa Nchini humo.

Leave a Comment