×

Jamii Yatakiwa Kuungana Kupinga Ukatili kwa Wanawake na Watoto

Afisa Program ya Harakati na Ujenzi wa Nguvu za Pamoja (TGNP) Anna Sangai, akitoa somo kwa wahudhuriaji. 

Kuelekea siku maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kati ya Novemba 25 hadi Desemba 10, mwaka huu, jamii imetakiwa kuungana ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Vitendo vya ukatili wa kijinsia vinatajwa kuwa na athari nyingi kwenye jamii ikiwemo kurudisha nyuma maendeleo ya mtu mmojammoja.

Wadau wakipata somo.

Akizungumza kwenye Semina ya Jinsia na Maendeleo (GDSS) inayoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Ofisa Program ya Harakati na Ujenzi wa Nguvu za Pamoja, Anna sangai anasema ili kupinga ukatili wa kijinsia, mabadiliko yanaanza kwa kila mwanajamii kutomeza ukatili wa kijinsia.

Wadau wakisikiliza kiumakini.

“Tunaanza kampeni tarehe 25, Novemba hadi tarehe 10, Desemba, kwa hiyo tuhakikishe hizi siku 16 tunazitumia ipasavyo katika kupinga ukatili unaoendelea kwenye jamii. Kutakuwa na maandamano ya amani ambayo yanaadhimishwa kwa kupaza sauti kupinga ukatili kwa namna mbalimbali ili kufikisha ujumbe kwa jamii, kuhakikisha nguvu inaongezeka katika jamii ili kupinga ukatili wa aina zote mfano, ukeketaji, haki ya afya na uzazi, ndoa za utotoni, ubakaji, ulawiti na itaongozwa na machampioni wenye ushahidi wa maandishi.

Somo likiendelea.

“Kutambua kamati za ulinzi za mtoto katika jamii na jinsi zinazofanya kazi, ni sehemu ambayo inatoa jukwaa la wanajamii kuzungumza changamoto zinazotokea kwenye jamii na kupanga mikakati ya kupambana na ukatili dhidi ya watoto ili kutengeneza nyenzo ambazo zitahamasisha serikali kutimiza kutokomeza ukatili,” Alimaliza kusema.

Leave a Comment