×

Yanga Yaibua Upya Sakata la Morrison, Yatoa Tamko TFF – Video

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa kwa sasa una wasiwasi kuhusu kesi ya mchezaji wao, Bernard Morrison, huenda ikabadilishwa kwa kuwa dirisha dogo la usajili linakuja na hakuna walichopokea kuhusu malalamiko yao.

 

Mwanzoni mwa mwezi Oktoba, mwaka huu, Yanga waliripoti kwamba Morrison mkataba wake haujakamilika kwa kuwa kuna sehemu hazijajazwa na wahusika, jambo linalomaanisha kwamba mkataba wake ni feki.

 

 

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, amesema kuwa wana mashaka na kesi yao hiyo ambayo haijaskilizwa, huenda mabadiliko yakafanyika kwenye mkataba wa dirisha dogo la usajili ukifika.

 

 

“Kesi yetu kuhusu Morrison tulipeleka malalamiko kwa wahusika na mpaka sasa hakuna tulichokipata, wasiwasi wetu ni kwamba ikifika Desemba 15 dirisha dogo la usajili likifunguliwa huenda wakafanya mabadiliko.

 

 

“Kwenye mkataba wa mchezaji Morrison sisi tuliweka wazi kwamba kuna sehemu hazijajazwa, hivyo huenda wakatumia mwanya huo kwenye dirisha dogo kuziba mapengo.  Maombi yetu ni kwamba shauri letu lisikilizwe na lifanyiwe kazi,” amesema Mwakalebela wakati akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya Yanga.

 

Leave a Comment