×

Wachoma Moto Bunge Kupinga Bajeti

MAMIA ya waandamanaji wanaopinga Serikali ya GUATEMALA wamechoma moto sehemu ya jengo la Bunge wakipinga Bbjeti iliyopitishwa siku chahe zilizopita na kutaka Rais Alejandro Giammattei ajiuzulu.

Wapinzani wamesema bajeti hiyo imepuuza athari za kiuchumi kutokana na #COVID-19 huku ikitoa kipaumbele kwa miradi mikubwa ya miundombinu kusimamiwa na kampuni zenye mahusiano na serikali.

Ijumaa iliyopita Makamu wa Rais, Guillermo Castillo, alionyesha kutokubaliana na bajeti hiyo akisema yeye pamoja na rais wanapaswa kuachia madaraka kwa manufaa ya taifa.

 

Leave a Comment