
JUMUIYA ya Umoja wa Ulaya (EU) imetoa wito kwa Serikali ya Marekani kusitisha utekelezaji wa hukumu ya kifo iliyoanza kutekelezwa tena kufuatia uamuzi uliochukuliwa.
Peter Stano ambaye ni Msemaji wa Kamati ya EU, amesisitiza kuwa EU inapinga vikali hukumu ya kifo kwa sababu ni hukumu ya kikatili inayokiuka #HakiZaBinadamu na haiwezi kusawazisha makosa ya mtuhumiwa baada ya utekelezaji.
Baada ya uamuzi kuhusu hukumu ya kifo kurejeshwa tena mwezi Julai, Serikali ya Marekani tayari imetekeleza hukumu hiyo kwa watu wanane na wengine watatu watauawa Desemba 11 mwaka huu.