×

Jay Z Aanza Rasmi Biashara ya Bangi

Moja ya kuifahamu leo November 26, 2020 ni Mwanamuziki maarufu nchini Marekani Jay-Z ametajwa kama ‘Afisa Mkuu mpya wa kampuni kubwa mpya ya bangi ya TPCO.

 

Kwa Marekani bangi ni halali katika majimbo kadhaa ikiwemo California, ambapo sasa ni biashara kubwa. Jay-Z ataongoza mikakati ya kampuni ya TPCO na kuhamasisha wasanii wengine mashuhuri kukuza biashara hiyo.

 

Jay Z amepata shavu kutoka kampuni kubwa ya utengenezaji na uzalishaji wa bangi iitwayo Caliva.

 

Mwaka jana Jay Z alipewa nafasi ya kuwa mkurugenzi mkuu wa mipango na mikakati wa kampuni hiyo , na kuingia ubia huo wa kufanya nao kazi kwa mwaka mmoja.

 

Katika nafasi hiyo Jay Z alikuwa akisaidia masuala ya ubunifu, maamuzi , juhudi za ufikiaji malengo na mikakati. Pia haki za kijamii kwenye mambo ya kuhahalilsha bangi, ikiwa pamoja na utetezi, mafunzo ya kazi, kuajiri wafanya kazi, na kufanya kazi kwa maendeleo.

 

“We want to create something amazing, have fun in the process, do good and bring people along the way,” Alisema Jay Z akimaanisha kuwa, anataka afanye kazi kwa usahihi katika ngazi za juu, akitumia uwezo wake wote katika sekta hii ya biashara ya bangi, jitihada bora za kitaalamu katika kuiendesha, na kubuni kitu cha kushangaza, na kufanya vizuri ili kuleta watu katika njia sahihi.

SOMA ==> Jay Z Ageukia Biashara ya Bangi

 

 

Leave a Comment