×

Standard Chartered Waungana na Sanlam Tanzania Kuanzisha Bima

BENKI ya Standard Chartered kwa ksuhirikianana kampuni ya bima ya Sanlam Tanzania, Januari 27, 2020 imezindua bidhaa mpya ya bima itakayogusa mambo mbalimbali ikiwamo nyumba na magari.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa bidhaa hizo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki Standard Charted, Sanjay Rughani, alisema kwamba benki hiyo imefurahi kuanzisha huduma hiyo muhimu katika ukuaji wa sekta ya fedha nchini.
Alisema ushirikiano kati ya benki na makampuni ya bima katika utoaji wa huduma hiyo una faida kubwa kwa wateja kwani unafungua njia ya udhibiti wa majanga ambayo hayakutarajiwa.


Bw.Rughani pia alipongeza utaratibu ulioelekezwa mwaka jana na Mamlaka ya Bima nchini (Tanzania Insurance Regulatory Authority) na Benki Kuu nchini kwa ajili ya mabenki na taasisi za kifedha, na kusema zinaonesha ni kwa namna gani mamlaka hizo mbili za udhibiti zinashirikiana na taasisi nyingine kukuza sekta.

Rughani alisema kwamba kuwapo kwa bima kumemaanisha kuangaliwa kwa mahitaji ya usalama wa mali.
Alisema kwamba kuzinduliwa kwa huduma hiyo kumelenga kuondoa maisha ya shaka ya wateja wake na pia kulinda rasilimali na utajiri wao.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Benki cha Wateja wa Rejareja, Ajmair Riaz, alisema kwamba kuanzishwa kwa huduma hiyo ni matokeo ya kusikiliza na kutekeleza maoni ya wateja wao nini wanakihitaji.


Bw.Riaz alisema utafiti uliofanywa na benki hiyo umeonesha kwamba wateja wake wanataka vitu wanavyoweza kuvimudu, urahisi wa kuvichukua, usalama na maisha yenye furaha.

Anasema wadau wao wanataka si usalama wao tu bali na usalama wa mali zake.
Bw.Riaz alisema benki hiyo ilifanyakazi kwa karibu na kampuni ya Sanlam Tanzania kuja na huduma hiyo ya pekee na ambayo wateja wake wataimudu na kuifurahia.

Alisema bima hiyo inashughulikia na masuala anuai kuanzia wizi wa magari, bima ya ajali na pia inawalinda wasaidizi waliokata bima akiwamo wasaidia wa nyumbani.

Akizungumza bima ya nyumba Bw. Riaz alielezea haja ya uwekezaji mkubwa wa makazi yao kuwa na utamaduni wa kuwekewa bima makazi yao dhidi ya hasara ya aina yoyote.

“kama benki tunatambua umuhimu wa makazi. Tunajua kwamba watu wanahangaika karibu nusu ya maisha yao kuwa makazi yao wenyewe. Wengi wananunua nyumba au wanajenga. kazi ya ujenzi au ununuzi inavuka mamilioni ya shilingi. hakika kwa uwekezaji huu mtu anatakiwa kujihadhari kwa kukatia bima dhidi ya majanga mbalimbali.” anasema Bw. Riaz.

Bw. Riaz alisema bima wanayoendesha wao ina mambo mengi yenye manufaa ikiwamo mkata bima kurejeshewa gharama zake za hoteli kama amepata ajali kilomita 30 kutoka nyumbani kwake, au anatakiwa kuwa katika eneo la ajali kwa siku zaidi, utekeji wa magari na kulazimishwa kutoa hela katika mashine za pesa kwa mkataba bima na kurejeshewa gharama za kuvutwa kwa gari ambalo limekatiwa bima.

Kutibiwa kwa mkataba bima wakati wa ajali au abiria waliokuwamo katika gari la mkata bima.
Pia kupatiwa fedha kiasi cha sh 50,000 kutumika kwa ajili ya usafiri wakati lililopata ajali linatengenezwa.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam, Bw. Khamis Suleiman, alipongeza ushirikiano wa kampuni yake na benki hiyo na kusema kwamba ushirikiano huo utaweza kuwafikishia watu wengi huduma ya bima.

Alisema ukataji bima unasaidia mtu kulinda rasilimali zake na kuhakikisha kwamba hazipotei kupitia majanga mbalimbali.

Alisema katika utengenezaji wa utajiri hakuna njia ya mkato ambayo haitakuumiza kwa hiyo ni vyema kuhakikisha kwamba mali zinawekewa bima dhidi ya majanga mbalimbali yakiwemo ya asili ambayo hayatabiriki.

Na Mwandishi wetu

Leave a Comment