
KAMPUNI ya New Habari 2006 LTD inayozalisha magazeti ya Mtanzania, Rai, Bingwa na Dimba, leo Desemba 5, 2020 imetangaza kusitisha uzalishaji kuanzia Jumatatu, Desemba 7 kutokana na mwenendo mbaya wa biashara.
Mhariri Mtendaji wa kampuni hiyo, Dennis Msacky, ameyasema hayo wakati akizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo na kusisitiza kuwa kuanzia Jumatatu Desemba 7, hakutakuwa na uzalishaji kabisa.