
MABONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’ na Twaha Kiduku wanatarajiwa kupanda ulingoni Desemba 26, mwaka huu katika mapambano ya usiku wa mabingwa yatakayopigwa ndani ya Ukumbi
wa Next Door uliopo Masaki jijini Dar.
Mbali ya mabondia hao, wengine wanatarajiwa kuwa ni Mfaume Mfaume, Tonny Rashid, Ismail Galiatano, Issa Nampepeche.
Seleman Kidunda, Baina Mazola, Haidari Mchanjo, Juma Choki na Loren Japhet Akizungumza na Championi
Ijumaa, mratibu wa mapambano hayo, Chris Mahundi, alisema kuwa mabondia hao watazichapa na mabondia kutoka nje ya Tanzania kwa lengo la kuonyesha ukubwa wa siku hiyo ya mabingwa.
“Hii itakuwa kubwa kuliko ambayo itafanyika ndani ya Next Door baada ya kumalizika kwa Dar Boxing Derby, siku hiyo kutakuwa na mapambano ya kimataifa ambayo yatakuwa ni moto wa kuotea mbali kwa sababu Twaha
Kiduku atacheza na Guy Tshimanga Tshitundu kutoka DR Congo, Mfaume Mfaume atazichapa na Chikondi Makawa
wa Malawi.
“Lakini Dullah Mbabe atamaliza ubishi na Simon Tchetcha wa Malawi, Tonny Rashid atazichapa