The House of Social Media
gunners X

Husna Amshushia Nai Tuhuma Nzito

0

husna

MREMBO aliyejipatia umaarufu Bongo kupitia mashindano ya urembo ya Miss Tanzania miaka ya nyuma na u-video vixen, Husna Maulid amemshushia tuhuma nzito msanii chipukizi wa Bongo Fleva, Nai.

 

Husna amedai kuwa, Nai alikuwa akimtongoza mzazi mwenzake huku akijua fika kwamba ni shemeji yake katika mahojiano maalum na Gazeti la IJUMAA, Husna amedai kuwa, alikuwa akijaribu kumpigia simu, lakini matokeo yake amekuwa akimjibu mbovu na kumtukana, jambo ambalo lilimkera na kuamua na yeye amuweke wazi kwenye mitandano ya kijamii.

 

Husna anasema kuwa, alifikia hatua ya kufanya hivyo kwa sababu alimuonya mno, lakini hakutaka
kusikia. “Yaani amekuwa ananishangaza sana, amekuwa akimtongoza baba mtoto wangu na kujipendekeza
mno kwake Nilimpigia simu kutaka kumwambia aache kumtongoza baba mtoto wangu, lakini hakusikia kabisa, badala yake akawa ananitukana,” anasema Husna.

 

Husna aliongeza kuwa, akiendelea kumsumbua baba mtoto wake, lazima ampe kichapo kwa sababu anaona kama wanazoeana bila sababu ya msingi na kwa nini amtongoze mwanaume wake na si wengine kwani wapo wa kuosha.
“Mimi ninapiga asikuambie mtu, sasa aendelee tu nitamuonesha.

 

Nitamtandika mchana kweupe na simuogopi,” anasema Husna Gazeti la IJUMAA lilimtafuta Nai ili ajibu tuhuma hizo kutoka kwa Husna, lakini simu haikupokelewa kwa muda mrefu hivyo jitihada za kumpa zinaendelea.

Stori: Imelda Mtema, Dar

 

Leave A Reply