
TIMU ya warembo 20 wanaowania Taji la Miss Tanzania 2020, wana jambo lao kesho ambapo patakuwa hapatoshi, warembo hao wenye mwonekano wa kuvutia watakuwa wanawania taji hilo ndani ya Ukumbi wa Julius Nyerere,Posta jijini Dar.
Shughuli ya kitoto kumpata mlimbwende atakayepeperusha taji la urembo kimataifa wakizungumza na Gazeti la IJUMAA walipotembelea chumba cha habari katika ofisi za Global Group zilizopo Sinza-Mori jijini Dar, mapema wiki hii, kila mmoja alitamba kulitwaa taji hilo.
Walisema kuwa, Jumamosi hii; leo Desemba 5, mwaka huu, itakuwa ni fainali ya kutafuta mrembo mmoja atakayewakilisha Tanzania katika mashindano ya Dunia ambapo shughuli hiyo itafanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere, (JNIC) uliopo Posta Dar, kuanzia saa 1:00 usiku hadi usiku mnene na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Spika amabye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson.