×

Wanigeria Wamuachia Ujumbe Mzito Sven Simba

ABDUL Maikaba, Kocha Mkuu wa Plateau United, amefichua kuwa Simba wana timu nzuri katika michuano hiyo lakini amemtaka kocha mkuu wa timu hiyo, Sven Vandenbroeck kuhakikisha anafanya mabadiliko ya kiufundi ikiwa anataka kufika mbali katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Maikaba ametoa kauli hiyo baada ya timu yake kuondolewa katika hatua ya awali ya michuano hiyo kufuatia Simba kupata ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza kabla ya Jumamosi kutoka suluhu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Maikaba alisema kuwa Simba wana kikosi kizuri lakini bado kinahitaji mbinu za kiufundi zaidi ili waweze kufanya vyema katika michuano hiyo.

 

“Nadhani haikuwa bahati kwetu japokuwa kabla ya mchezo kulikuwa na mambo mengi ya hujuma lakini tulifanikiwa kuyashinda ila hatukuweza kupata matokeo katika mchezo wetu hivyo tumeondolewa kwa bao la ugenini.

 

“Nawapongeza Simba kwa kufuzu hatua inayofuata lakini bado inahitaji kuufanyia kazi upungufu wake kwa sababu imekuwa ikicheza mpira wa taratibu ambao ni hatari kama watakutana na timu ngumu zaidi kwa sababu nilitegemea upinzani mkubwa kutoka kwao ila haikuwa hivyo licha ya nafasi ambazo tulipoteza,” alisema Maikaba.

Ibrahim Mussa, Dar es Salaam

 

Leave a Comment