×

Marioo Akiri Kwenda Kwa Mganga

MSANII anayekuja kwa kasi kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva, Omary Mwanga ‘Marioo’ amesema ameshawahi kwenda kwa mganga ili kuweka mambo yake ya kimuziki sawa.

 

Akizungumza na AMANI, Marioo amesema anajilaumu kufanya hivyo kwani aliambulia kuwekwa chale bila kufanikisha chochote hadi leo.

“Niliwahi kwenda kwa mganga kwa ajili ya kuweza kuweka mambo yangu sawa lakini huwezi amini hakuna kitu nilichioambulia zaidi ya kuchanjwa chale mwilini, na hapo ndipo nilipoamini kwamba Mungu ndiye muweza wa kila kitu,” alisema Marioo ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya Mama Amina.

Stori: Khadija Bakari

MCHEKI!! PACHA wa MORRISON ALIVYOTAKA KUJIRUSHA kwa MASHABIKI “NITAONANA na MORRISON”

Leave a Comment