
MWANAMUZIKI milionea kutoka Bongo Fleva Diamond Platnumz, kwa mara ya kwanza ameingia kwenye chama cha watumiaji simu za iPhone, baada ya kununua iPhone 12 Pro ambayo ndiyo iPhone yake ya kwanza kutumia. Kama we’ ni mtumiaji sana wa Insta basi utakuwa unaona jinsi anavyotuonyesha macho matatu.
Diamond amekuwa mtumiaji wa Samsung kwa miaka mingi, sasa kaamua ku-upgrade na kuamua kuingia kwenye association of iPhone 12 Pro users.
Bado mzazi mwenziye, Zari, ambaye pia naye anaonekana kutoshoboka sana na matoleo ya iPhone yote yaliyowahi kutokea. Labda baada ya baba watoto kuhamia upande wa pili na yeye atabadili maamuzi. iPhone 12 Pro inauzwa kuanzia Sh. mil. 3.50 had mil. 4 za Tanzania.