×

Facebook Yakabiliwa na Kesi ya Kutaka ‘Kuua’

KAMPUNI ya #Facebook Inc inaweza kulazimishwa kuuza mali zake ikiwemo #WhatsApp na #Instagram baada ya Tume ya Biashara ya #Marekani kufungua mashtaka dhidi ya kampuni hiyo ikisema ilitumia mkakati wa “kununua au kuzika” kuwarubuni washindani wake.

 

Facebook inakuwa kampuni ya pili kubwa kwenye Uwanja wa #Teknolojia kukabiliwa na changamoto ya kisheria mwaka huu baada ya Idara ya Sheria ya Marekani kuishtaki Google Alphabet Inc mnamo Oktoba, ikiishutumu kutumia nguvu katika soko ili kujilinda na washindani.

 

Kesi hiyo iliyofunguliwa Jumatano inaishutumu Facebook kwa kuwanunua wapinzani, ikiwemo Programu ya Picha (Instagram) kwa Dola bilioni 1 mwaka 2012 na Programu ya Ujumbe (WhatsApp) kwa Dola milioni 19 mwaka 2014.

Leave a Comment