TECNO yaja na zawadi kwa wateja wake msimu wa sikukuu
Global Publishers December 10, 2020 0 Comments
SHARE THIS:
Erick Mkomoye ,Meneja mahusiano wa kampuni ya simu ya Tecno akizungumza na waandishi wa habari
Kampuni ya simu za mkononi ya TECNO imekuja na zawadi za msimu wa sikukuu kurudisha kwa wateja wao.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa promotion ya mwezi mmoja Erick Mkomoye amesema kuwa wameamua kuja na zawadi hizo ili kurudisha furaha kwa wateja wao ambao wamekuwa pamoja nao.
“Kama tujuavyo simu ambazo zipo sokoni kwa sasa na zimefanya vizuri ni CAMON 16 s ambayo ina Gb 128 ambayo unaweza ukaweka kumbukumbu zako ikiwemo vodeo, picha na nk na ina uwezo wa kufanya kazi kwa uwezo mkubwa.
Meneja Masoko wa TECNO William Motto akizungumza na waandishi wa habari
” Na Spark 5 ambazo ina GB 64 battery yenye uwezo wa kudumu na chaji kwa muda mrefu na zinapatikana kwenye maduka yote ya TECNO Tanzania nzima kwa hiyo wateja wetu wapite katika maduka hayo ili wanunue na kujipatia zawadi kemkem, “amesema.
Nae meneja masoko wa TECNO William Motto amesema kuwa kila mwaka huwa wanakuwa na zawadi ili kurudisha furaha kwenye familia za wateja wao.
” Kuna zawadi nyingi ambazo msimu huu wa sikukuu kuanzia tarehe 8 Desemba mpaka 13 Januari tutakuwa tunatoa zawadi kwa wateja wetu ikiwemo mashine ya kufulia, Flat screen smart kubwa kwa ajili ya familia, blenda, jagi, rice cooker na vingine vingi na hivi utavipata ukinunua simu hizo.
“Tunarudisha furaha nyumbani wateja wetu wapite maduka yetu yaliyopo Tanzania nzima wanunue na kujipatia zawadi hizo,