
Kampeni ya ‘Chanja Kijanja na Exim Mastercard’ inayolenga kuhamasisha wateja wabenki hiyo kutumia kadi katika manunuzi ya mtandaoni au kufanya malipo kupitiamashine za malipo (POS) imechukua sura mpya huku zawadi kwa washindi mbalimbaliwa kampeni hiyo zikiongezwa.
Kampenihiyo inatoa fursa ya kipekee kwa wateja wa benki hiyo kufurahia hudumazinazokwenda sambamba na mfumo wa maisha yao kupitia benki hiyo.
Kwamujibu wa mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na kati wa Benki ya Exim Tanzania,Bw. Andrew Lyimo, alisema kupitia kampeni hiyo washindi sasa watajipatia zawadimbalimbali ikiwemo pesa taslimu za ada ya shule kwa mtoto pamoja na vifaa vyotevya shule.
“Kwakuheshimu vipaumbele na matakwa ya washindi wetu, kupitia kampeni hii sasatunatoa uhuru kwa washindi watatu wajichagulie wenyewe zawadi zao ikiwemo kwendaSerengeti au kwenda visiwani Zanzibar wakiwa na wenza wao huku kila kitu kikiwakimelipiwa au hata zawadi ya pesa taslimu ya ada ya shule kwa mtoto mmojapamoja na vifaa vyote vya shule.’’ Alisema.
Alibainishakuwa wakati wa kampeni hiyo, jumla ya washindi 10 wa kila wiki watapata zawadiza vocha za manunuzi zenye thamani ya shilingi 50,000 huku kila mwezi washindiwatano (5) watazawadiwa simu janja (smartphones).
“Kamailivyokuwa awali, kutakuwa na zawadi za kila wiki, kila mwezi na kubwa zamwisho wa kampeni. Wanachotakiwa wateja wetu ni kufanya miamala yao kupitiakadi ya Exim Bank MasterCard mara nyingi iwezekanavyo kwa kuwa kila muamalaunaongeza nafasi moja ya kushinda,” aliongeza.
Kwamujibu wa Bw. Lyimo, Kampeni hiyo ipo wazi kwa wateja wote wanaomiliki kadi zaExim Bank MasterCard, pamoja na wateja wote ambao wameomba au wataomba kadimpya katika kipindi cha kampeni.
“Kwaupande wetu Benki ya Exim, wateja wanaotumia kadi zetu wamekuwa wakifurahiaurahisi wanapofanya manunuzi au malipo kwenye ya mahitaji muhimu kwenye maduka(Shopping), ununuzi wa bidhaa kimataifa kupitia mtandaoni mfano Amazon, Ebay,Alibaba, Jumia, Kikuu, Duka direct, malipo wakati wa safari, malipo ya hoteli nashughuli za kitalii. ” Alisema.
NayeMkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo Bwana Stanley Kafu, alielezeakufurahishwa kwake na mwitikio mkubwa wa kampeni hiyo akisema, “Tumefurahishwasana na mapokeo ya kampeni ya Chanja Kijanja. Maboresho tuliyoyafanya kwenyekampeni hii yanasadifu ubora wa huduma za kibenki kwa wateja wetu, na hiyo ndiofalsafa ya kiutendaji hapa benki ya Exim” alisema.
Dar es Salaam; Disemba 10, 2020