×

Kisa Simba, Kocha FC Platinum Ameapa Kuitoa Simba

KOCHA wa FC Platinum ya Zimbabwe, Norman Mapeza amefunguka anatambua ugumu katika mchezo wao wa Hatua ya Kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba lakini ameapa kuhakikisha wanapata matokeo ya ushindi katika mchezo wa kwanza kabla ya kuja Tanzania.

 

Mapeza ambaye ameichukua FC Platinum hivi karibuni baada ya kutimuliwa kwa aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Piere De Jong raia wa Uholanzi kutokana na kukosa sifa za kukaa kwenye benchi la ufundi timu hiyo kwa mujibu wa sheria za Shirikisho la Soka Afrika (Caf) huku akishinda mchezo wa hatua iliyopita kwa jumla ya mabao 4-1.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mapeza alisema kuwa naamini mchezo wao na Simba hautakuwa rahisi lakini atahakikisha wanapata matokeo mazuri katika mchezo wa kwanza kabla ya kuja Dar es Salaam ambapo wapinzani wao wanategemea kucheza mbele ya mashabiki tofauti na wao.

 

“Najua haitakuwa kuwa mechi rahisi kwetu , tunaanzia nyumbani na kitu kikubwa kwetu ni kuhakikisha timu inapata matokeo, tayari tupo katika maandalizi licha ya kuwepo na mvua za kubwa huku kwetu lakini tumekuwa tukiwafuatilia wapinzani wetu.

 

“Ninachokiangalia ni kwa jinsi gani naweza kupata matokeo mazuri nyumbani kwa sababu najua hapa kwetu bado Corona inatusumbua, hivyo hatutakuwa na mashabiki na itapunguza hali kwa kiasi fulani tofauti na Simba ikiwa kwao inacheza mbele ya nusu ya mashabiki wake,” alisema Mapeza.

Stori na Ibrahim Mussa,dar es Salaam

Leave a Comment