
KIM KARDASHIAN amempoteza mtu aliyekuwa miongoni mwa aliokuwa akiwatetea kwenye kesi zao mahakamani. Brandon Bernard amenyongwa hadi kufa Jana mjini Texas Marekani.
Haikuwa siku nzuri kwa Kardashian ambaye kwa muda mrefu alipambana na kesi hiyo ya mauaji akiiomba mahakama kumpunguzia adhabu Brandon kwa kuwa ana familia.
Bernard aliua watu wawili (Todd na Stacie Bagley) mwaka 1999 akiwa na umri wa miaka 18, baada ya wenzake kuwaua kwa risasi, Brandon aliingiza miili hiyo kwenye gari na kuiwasha moto.
Kardashian alikutana na pingamizi kali kutoka kwa ndugu wa marehemu. Lana Ladd alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha Brandon anauawa pia, huku akimshukia Kardashian kwa kumwambia hana uchungu kwa sababu waliouawa siyo ndugu zake.
“Kim Kardashian inabidi aache kujaribu kumsaidia muuaji Brandon Bernard kwenye adhabu ya kunyongwa kwa sababu hapati maumivu kwa familia aliyoiharibu [Brandon],” alisema Lana. Brandon alinyongwa jana mishale ya saa 9:27 usiku kwa saa za Marekani.