
Mbunge wa Jimbo la Buchosa kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Eric Shigongo James, mapema leo Ijumaa Desemba 11, 2020, ameshirikiana na wananchi wa Kijiji cha Mizolozolo katika ujenzi wa daraja lililokuwa limesombwa na mvua kubwa iliyonyesha mwishoni mwa mwezi uliyopita.
Kubomoka kwa daraja hilo kuilisababisha adha kubwa kwa wakazi wa jimbo hilo, kiasi cha kumlazimu mbunge huyo kujenga njia mbadala kwa mawe, ambapo ilitatua shida ya kukwama kupitia kwa magari kwa muda mfupi, jambo ambalo sasa limemfanya kulazimika kujenga daraja la kudumu linalotarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Machi mwaka huu.
Awali, kabla ya kufika katika ujenzi wa daraja hilo, Shigongo alipata fursa ya kutoa msaada wa mabati 30 yaliyokuwa yamepelea kwenye ujenzi wa msikiti mpya katika Kijiji cha Bukokwa, ambayo yalipokelewa na Shekhe Bashiru Kabanga, huku akiwaahidi waaumini wa msikiti huo kuendelea kushirikiana nao katika ukamilishaji wa ujenzi wa eneo lililobaki.