×

Manchester Derby Kutikisa Old Trafford Leo

UWEPO wa Sergio Aguero hata kama atakuwa katika benchi katika mechi ya Manchester Derby utakuwa na faida kubwa kwa timu yake ya Manchester City itakayo kipiga dhidi ya Manche ster United.

Kauli hiyo imesemwa na beki wa zamani wa Man City, Joleon Lescott.

 

Aguero amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara ambapo yamemuweka nje kwa muda mrefu, lakini alirejea uwanjani Jumatano ya wiki hii na kufunga bao katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Marseille katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

 

Lescott amesema kuwa safu ya ulinzi ya United ikiwa chini ya Harry Maguire itakuwa na hofu kuona Aguero akirejea kazini.

Kocha wa City, Pep Guardiola amesema kuwa straika wake huyo hatakuwa tayari kwa ajili ya kucheza mchezo huo wa leo unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Old Trafford.

 

Lescott amesema: “Naamini atahusika katika kucheza, yeye na Wayne Rooney wamefunga mabao mengi katika derby hii.“United wakimuona kwenye benchi watakuwa wanajua kazi ipo, (Aguero) anafurahia sana kufunga, hata kama ataingia wakiwa wanaongoza 2-0 bado atakuwa na kiu ya kufunga.”

 

Aguero ameshafunga mabao 9 katika mechi dhidi ya wapinzani hao akishika nafasi ya tatu kwa waliofunga mabao mengi katika derby hiyo.

Leave a Comment