×

Marioo Amjibu Harmonize

MSANII Marioo ameipinga kauli ya msanii na ‘boss’ Wa lebo ya Konde Gang, Harmoniz,e kwa kusema wimbo wake wa ‘Ushamba’ ndiyo wimbo bora kati ya nyimbo zote zilizotoka mwezi Novemba.

 

Marioo amesema wakati Harmonize anatoa kauli hiyo wimbo wake ‘Mama Amina‘ ulikuwa haujatoka ila Ungetoka asingeweza kusema hivyo.

 

“Wimbo wangu umetoka mwezi wa kumi na moja una wiki sasa, kipindi kile anasema hivyo wimbo wangu ulikuwa bado haujatoka na kama ungetoka sidhani kama angeweza kuongea vile.  Dude langu hili ni ‘hit song’ na la moto kuliko magoma yote yaliyotoka sasa hivi,” amesema Marioo.

Leave a Comment