×

Antony Joshua Amtwanga Pulev kwa KO

BONDIA Anthony Joshua wa Uingereza amefanikiwa kutetea mataji yake ya ndondi, kwa kufanikiwa kumchapa kwa knock-out bondia Kubrat Pulev katika raundi ya 9 ya mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Wembley na kushuhudiwa  na watazamaji Elfu Moja pekee, ikiwa ni sehemu ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa COVD 19.

 

Joshua mwenye asili ya Nigeria, ametimiza ushindi wa 24 katika mapambano 25 aliyopigana, mapambano 22 kati ya hayo akishinda kwa knock-out, Bondia huyo kwa sasa anashikilia mikanda minne ya uzito wa juu (Heavyweight Title) WBA (Super), IBF, WBO, na IBO.

 

Joshua  anatarajiwa kupambana na Muingereza mwenzie Tyson Furry katika kipindi cha miezi 12 ijayo.

Leave a Comment