×

Daraja la Busisi Lapewa Jina la Rais Magufuli

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale, leo Desemba 16, 2020 amelibadilisha jina Daraja la Busisi lililopo mkoani Mwanza na kuliita JP Magufuli Bridge mara baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wake.

 

Ujenzi wa daraja hilo unatekelezwa na kampuni ya China Civil Engineering Group Limited kutoka nchini China na litakuwa na urefu wa kilometa 3.2 ambapo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika mnamo mwaka 2024.

Leave a Comment