
MBUNGE wa Buchosa, Eric Shigongo amemtembelea mtoto Rashid ambaye Desemba 11, 2020 akiwa njiani kuelekea jimboni Buchosa eneo la Nyakasungwa alimkuta mtoto huyo kando ya Barabara akiwa anaumwa huku akitapika.

Baada ya kumsaidia mtoto huyo ambaye kwa sasa anaendelea vizuri, Shigongo ameahidi kumsomesha mtoto Rashid ili aweze kutimiza ndoto za maisha yake.